Thursday, May 23, 2013

MABAKI YA SILAHA ZA LIBYA YANATUMIKA VIBAYA AFRIKA

Umoja wa Mataifa umesema makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, yanatumia mabaki ya silahi zilizotumika Libya mwaka 2011 kwa ajili ya kuulia tembo. Ripoti iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon inasema kuwa biashara ya meno ya tembo inatishia usalama wa wanyama hao hasa katika nchi za Cameroon, Chad, Gabon na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ban amesema kuwa kuna uwezekano biashara haramu ya meno ya tembo ikawa ni chanzo cha mapato kwa vikundi vyenye silaha katika ukanda huo. Ripoti ya Katibu Mkuu wa UN imegusia pia silaha za Libya kutumiwa na jeshi la Joseph Kony la LRA ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataiafa ya Jinai ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Joseph Kony na makamanda wake wanatuhumiwa kuwatumia watoto wadogo kama wapiganaji katika jeshi lake ambapo jeshi hilo limekuwa likipigana na serikali ya Uganda kwa miongo miwili sasa, kabla ya kufurushwa kutoka katika ngome yao, Kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO