Friday, November 25, 2011

CHANGAMOTO KWA WAISLAM VYUONI

Assalam alaykum warahmatul lahi wabarakatuh

Amma baada ya kumshukuru Allah (sw) na kumtakia Rehma na Amani Mtume wake Muhammad (saw) napenda kuchukua nafasi hii kulizungumzia suala moja tuu.

Kutokana na waislam kuwa nyuma katika kila kitu hatuna budi kuanza kubadilika kwanza  sisi vijana ili tuwe ndio miongoni mwa sababu za mabadiliko ya ndugu zetu wingine na hata wazee wetu.

Amma lengo kuu la uandishi huu ni kuanzisha suala moja tuu ambalo ni muhimu kwetu na muhimu kwa ndugu zetu hasa waliochini yetu kitaaluma. Suala lenyewe ni usaidizi kwa ndugu zetu hawa katika ufaulu wa mitihani yao ya kishule na ya kitaifa ili hatimaye waweze kuvuka kutoka ngazi moja ya kitaalkuma na ili waende nyingine na hatimaye wawezi kuingia vyuoni  nao pia wasaidie wenzao badala yetu.

Usaidizi huu naugawa katika sehemu kuu mbili ambazo ni :

        i.            Namna gani wataweza kwanza kuchagua kozi kulingana na uwezo wao wa ufaumu wa masomo husika.

      ii.            Namna gani wataweza kujibu mitihani yao/ kusoma ili kuweza kujibu mitihani yao

Lengo  kuu langu kwa kuzungumzia ni suala la pili ambalo ni namna gani tutaweza kuwasaidia wao kujibu mitihani  yao. Hapa walengwa wakuu ni wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kwani ndio wanaoongoza kwa kufeli na hukosa njia mbadala za kujiendeleza.

Hivyo namna ya kuwasaidia pia naweza kuigawa katika sehemu kuu mbili ambazo ni :

        i.            Kwanza kuanzisha tuition kwa ajili ya wanafunzi wa sayansi

      ii.            Kuanzisha pia vituo maalum kwa ajili ya kufundisha masuala mazima ya practical.

Hapa pia lengo langu kuu ni suala la pili ambalo ni kuanzisha vituo maalum kwa ajili ya mafunzo ya practical kwani tuition za masomo ya kawaida zipo nyingi kwa ajili ya waislam kama MSAUD na nyinginezo.

Katika chuo chetu kikuu cha Muhimbili tunarasilimali watu ambao wamefaulu katika kiwango ambacho wameingia katika gredi ya taifa. JE NAMNA GANI WANAFUNZI  HAWA WANAWEZA KUTUMIKA KWA AJILI YA KUWASAIDIA NDUGU ZETU WALIOCHINI ILI NAO KUPITIA UFAULU AU UELEWA ULIOTUSAIDIA SISI NAO WAWEZE KUVUKA KATIKA STAGE HIZO.?

Tukiwa kama waislam hatuna budi kusaidiana sisi kwa sisi ili na mwenyezimungu pia aweze kutushushia Rehma zake kwani ndugu zetu (makafiri) wana mbinu  mbalimbali ili nao waweze kunasuana katika elimu zao ambapo miongoni mwa mbinu hizo ni:

        i.            Kuanzisha vyuo mbalimbali ili walewanaofeli waweze kubebwa na hatimaye kuendelea sisi kama waislam hatuna zaidi ya kimoja walichotupa wao.

      ii.            Kuanzisha shule zao ili waweze kutumia mbinu zao kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa namna mbalimbali kama kuwapa mitihani na kadhalika na hatimaye kuongoza kwa ufaulu sisi hatuna shule na kama tunazo ni za mwisho kabisa.

    iii.            Kuanzisha taasisi ndogondogo  ambazo zina wajibu wa kusaidia wenzao sisi hatuna tasisi hata moja.

     iv.            Kupata misaada mbali mbali kutoka katika makanisa na misaada ya nje ya nchi ili tu waweze kufanikisha mambo yao sisi ni wenyewe tu na hatuna msaada wan je zaidi ya tende(ramadhan) na nyama (hijja).

       v.            Kugawa misaada mbali mbalimbali ili ya kielimu na kifedha katika mashule yao.

Katika mambo haya yote sisi kama waislam hatuna hata moja na hata kama tunalo basi halina uwezo ukilinganisha na wenzetu. Sasa kikubwa ambacho tunaweza kufanya kama waislam ni kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kupitia masuala yaliyoelezwa hapo juu.

Tukiwa kama wanafunzi wa kiislam kozi za sayansi tuna dhimma kwanza kwa elimu tuliyonayo hususani ambayo inaweza kuwasaidia ndugu zetu hawa wa elimu ya chini yetu ilinao waweze kunasuka na pia wasiweze kunasa/kujikwaa katika mashimo ambayo sisi tulijikwaa. Sasa nini ushauri wangu kutokana na haya yote.

Suala kuu ambalo ni lengo kuu la uandishi huu ni uanzishaji wa maabara maalum ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu hawa waliochini yetu. Suala hili linaweza kufikiwa iwapo tutakuwa na nia na pia kwa kufanya masuala yafuatayo:

        i.            Kufanya utafiti wa gharama za ununuzi wa vifaa vya kimaabara zikiwemo,

a)      Bansen barner,

b)      Test tubes,beakers, pipette, burette n.k

c)      Chemicals mbalimbali

d)      Na kadhalika

      ii.            Kutafuta eneo ambalo linaweza kutumika kwa ajili ya ufundishaji huu mfano eneo la wazi la msikiti wetu Muhimbili, kuomba eneo msikiti wa idirisa, kuomba nafasi msaudi  au eneo mbadala ambalo linaweza kutumika kama maabara japo kwa kuanzia

    iii.            Kushawishi watu ambao waliingia katika chuo hichi cha Muhimbili kwa matokeo mazuri zaidi  au kuomba msaada kwa vyuo vingine vya sayansi kama MSAUD inavyofanya.

Masuala haya yote yatafanikiwa tu kwa kuanza kufanya tathmini ya ngarama zote zikiwemo za ununuzi wa vifaa,  gharama ambazo wanafunzi wataweza kuchangia, watu ambao watajitolea kufundisha na eneo halitokuwa na utata.

Mwisho kabisa kama nilivyoanza ndugu zetu hawa makafiri wana mbinu mbalimbali za kuuangamiza huu uislam wetu uliobaki na tunaambiwa katika qur’an kwamba yaliyo nyoyoni mwao ni makubwa zaidi ya wayasemayo hivyo hatuna budi kuamka na kukunja mashuka tupambane lakini hatutoweza kupambana bila ya kuwa na vigezo mfano.

Tukitaka vyuo vyetu hatujasoma, tukitaka hospitali zetu hatuna madaktari, mahakama hatuna wanasheria wetu na hta vyombo vikubw vy habari hatuna waandishi. Hivyo yote haya yanahitaji sababu kwanza ili yafanikiwe.

Ni hayo ndugu zangu waislam sina zaidi tujifunge mkanda tuangalie uwezekano nao upo ni kuamua tu na hatuwezi kuamua mpaka tuwe na nia, na hatuwezi kuwa na nia mpaka tujue kuwa sisi ndio inabidi kuwa sababa nalo hatuliwezi mpaka tuwe na imani kuwa tuna dhimma kwa ndugu zetu  na tutaulizwa.

WABILLAHI TAWFIIK…..