Friday, November 25, 2011

FORM SIX NA FORM FOURASSALAM ALAYKUM WARAHMATUL LAHI WABARAKATU.
JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAM WA CHUO KIKUU CHA MUHIMBILI (MSAMU)
2011 - 2012

UTAMBULISHO;
Amma baada ya kumshukuru Allah (s.w)  na kumtakia Rehma na Amani mtume wetu na mjumbe wake Muhammad (s.a.w)  sisi ni wanafunzi wa chuo kikuu  cha Afya na utafiti  wa tiba cha MUHIMBILI (Dar-es-salaam) tukishirikiana na vyuo vingine .
      Tunapenda kuchukua nafasi hii  ya kuandika hii  nakala kwa ajili ya kuwafikishia ndugu zetu  wa chini yetu (form one hadi form six). Sisi kama wanafunzi /waislam tulio katika elimu ya juu ya chuo  tumeona kuwa tuna dhimma  ya kuwasaidia ndugu zetu  waliokatika kiwango cha chini cha elimu  ambao tunahisi kuwa yanaweza kuwasaidia/kuwa na umuhimu   katika masuala yao mazima ya kielimu.
Katika nakala hii  tumeamua  kiugawa katika vipengele vinne, ambavyo  ni; 
1.      Namna   ya kuiendea  mtihani katika maandalizi  yote  ya kivitendo  na kiimani
2.      Namna  gani utayapokea matokeo yako  kwa namna yoyote ile yatavyokuwa mazuri, mabaya au ya kati nakati
3.      Namna ya kujiunga katika vyuo vikuu hususani kwa chuo cha afya Muhimbili na vinginevyo(katika suala zima la kiafya)
4.      Hitimisho na ushauri

 1 ; MAANDALIZI YA MITIHANI
Katika kipengele  hiki cha maandalizi  ya  mitihani  na namna na yakujiandaa   kuuelekea mtihani  tumekigawa katika vipengele vikuu  vinne  kama ifuatavyo;

a.                     maana ya mitihani.
Mtihani ni kipimo   cha imani (kidini),  uelewa  au ufahamu wa mtu juu ya kitu  fulani   kwa mfano  Mwenyezimungu (s.w)  ametuandalia  mitihani  mbali mbali  kama maradhi  au vifo ili kutupima imani  zetu  kama tutafaulu au tutafeli.  Pia katika mashule yetu   imeandaliwa mitihani  ili kutupima ufahamu  uelewa  wetu juu   ya yale ambayo tunayasomea.
b.                     Namna ya kujiandaa  na mitihani
Katika namna ya kujiandaa na  mitihani  tumeamua kugawa katika namna kuumbili;
(i)                 Maandalizi ya kivitendo
    Katika maandalizi ya kivitendo mtu hujiandaa pale tu anapoingia katika  shule kutokana na  kufahamu kuwa ipo siku  atafanya mitihani na kumaliza shule. Mitihani hiyo ndiyo  ambayo itakufanya  uweze kufaulu na kwenda katika ngazi ya juu zaidi au kutokwenda.
Hivyo basi hatuna budi  kujiandaa kwa namna yoyote ile iwayo ili tuweze kufaulu  na kuweza kuendelea katika  ngazi za juu zaidi na hatimaye kuweza kutimiza yale malengo yetu.
(ii)               Maandalizi  ya kiimani.
    Katika maandalizi haya mtu  huanza  katika ngazi ya kifamilia, kuanzia pale unapozaliwa  hadi kufikia kiwango cha kuweza kujitegemea  kwa maisha yako na hatimaye kuwa baba au kuwa mama.
 Hivyo hatuna budi basi  kuamini kuwa  mitihani nikipimo  cha  kuamini Qadar (kheri au shari ) zinatokana na  Mwenyezimungu (s.w). Hivyo basi  hatuna budi kuelewa kuwa tunadhimma  ya kutekeleza yale yote  ambayo ndiyo sababu  ya sisi kufaulu au kufeli  katika mitihani hiyo (KIIMANI)
Hivyo katika maandalizi haya   hatuna budi  kuiendea  mitihani yetu katika namna  ambayo Mwenyezimungu (sw)  ataipendelea ambayo ni;
Ø   kusimama   visimamo vya  usiku,
Ø  Kuingia katika chumba  cha mtihani  haliyakuwa tumetia udhu,
Ø   Kuwahi katika eneo la tukio (chumba cha mtihani)  ili kuyazoea mazingira  ya eneo husika,
Ø  Kumtanguliza Mwenyezimungu kwa kusoma  suratul fat-ha(quran 1) na suratul muadhwatain (falaq& nnasi)  mwisho ni saratul ikhlas ni vizuri idadi ya witri ikiwezekana.
Ø  Kumsabahi Mwenyezimungu kwa nyiradi mbalimbali (fupifupi).
iii.        namna ya kujibu mtihani
Katika kujibu  mtihani mambo ya  msingi  ya kuzingatia  ni kama ifuatavyo;
Ø  Kuanza na swali unalolijua  ambalo pia ni lenye  alama nyingi(marks)
Ø  Kutumia uwezo wako wote katika  kulijibu  swali ambalo unalijua
Ø  Kwa swali ambalo huna uelewa nalo  kabisa ni vizuri  usilifanye   na uliache kwani utapolifanya  utaonyesha  udhaifu wako  kwa wasahilishaji au ulifanye mwisho baada ya maswali yote  unayoyafahamu kuyafanya.
Ø  Ni vizuri  kufanya maswali yote kama unayaweza na muda upo mfano mtihani wenye maswali kumi na mbili 12 basi fanya yote  kumi na mbili
Ø  Ni vizuri pia kuwa makini na muda wa kufanya mtihani kwani muda ni s ehemu pia katika mtihani

2. NAMNA YA KUYAPOKEA MATOKEO YETU
Matokea ni zao au chumo ambalo hutokea baada ya kufanyika kwa jambo fulani ,hivyo machumo yaweza kuwa ni kuridhisha au kutoridhisha.
Hivyo matokeo ya mitihani yetu yaweza kuwa ni mazuri , ya kati na kati au yasiokuwa mazuri.
1.        MATOKEO MAZURI;
Hayo ni matokeo ambayo mtu huyapata yakamuwezesha yeye/wewe kwenda katika ngazi ya juu ambayo anaitarajia/ unatarajia.
Watu wengi wapatapo matokeo  mazuri hupata kiwewe kutokana na furaha waliyonayo  na kukurupuka na kushindwa kufanya uamuzi uliosahihi.
La umuhimu nikumuomba Mwenyezimungu na kumshukuru na kutafuta ushauri kwa wale walio juu  yako ni lipi la kufanya kabla ya kufanya uwamuzi.  
2.      KATI NA KATI
Haya ni matokeo ambayo mtu hupata alama/matokeo  mazuri lakini kutokana na alama hizo hazikumuwezesha yeye kupata kuisoma kozi ambayo ameitarajia. Mfano mtu ambaye amepata gredi ya tatu (Division iii) na ametaka asome udaktari (medicine). Muhimbili . Ni ngumu kupata kozi hiyo lakini kuna baadhi ya vyuo ambavyo anaweza kupata chuo kutokana na alama hizo. Hivyo  basi ni uzuri kutafuta ushauri kupitia wanafunzi/waislam walio vyuoni ili kuweza kumshauri cha kufanya..
3.      MABAYA (YASIYORIDHISHA)
Haya ni matokeo ambayo hayatamuezesha mtu kujiunga, kuingia elimu ya juu (vyuo) katika kiwango cha shaada(degree) maranyingi watu hawa huwa ni wenye kukata tamaa na wengine kuamua kurudia mtihani ili waweze kufaulu hali yakuwa kuna njia nyingine              (mbadala) ambazo wanaweza kupitia na kufikia malengo yao mfano ASTASHAHADA (CERTIFICATE), STASHAHADA (DIPLOMA),  na hatimae kufikia SHAHADA (DEGREE)  na kisha  kuendelea ngazi au kiwango  cha juu zaidi kielimu.

USHAURI
     Tusingependa kumshauri mtu arudie mtihani kwa maana utafiti umeonyesha kuwa wengi wanaorudia mtihani hawafanyi vizuri,Hivyo ndo maana tumetoa nakala hii kuonyesha kuwa njia mbadala ambayo ni zaidi ya kwenda kusomea ualimu.
Lakini kwa wenye kuamua mitihani yawapasa wafanye yafuatayo kwanza:
        i.            Kufanya tathmini ya kina sababu zilizopelekea matokeo yake kuwa hivyo
      ii.            Je sababu hizo zinatatulika kirahisi
   iii.            Basi atatue matatizo hayo ndio aweze kurudia mtihani
Miongoni mwa sababu zinaweza kuwa;
a)     Sababu za ndani/binafsi (internal factor)
b)    Sababu za nje (external factors)
Sababu zote hizi mwisho wa siku huchangia katika kuleta matokeo ama mazuri au mabaya, zinaweza kuwa za kiuchumi, kifamilia, kimazingira, kijamii au kitaasisi (shule).
Baada ya kutatua hizo sababu tunaweza kukubaliana na wewe katika mawazo yako ya kurudia mtihani wako.

SOME OF THE FACULTIES WITH THEIR RELATED
UNIVERSITIES AND COLLEGES.
-ALLIED HEALTH SCIENCE;
        I.            Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) HK University Private Dar es Salaam
      II.            International Medical and Technological University (IMTU) IM University Private Dar es Salaam
    III.            Kilimanjaro Christian Medical College (KCMC) KC University College Private Kilimanjaro
    IV.            Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) MH University Public Dar es Salaam
      V.            Weill Bugando University College of Health Sciences (WBUCHS) BU University College Private Mwanza.
    VI.            All universities under Ministry of health

-BUSINESS;
        i.            College of Business Education (CBE) Dodoma CBD Non-university Public Dodoma
      ii.            .College of Business Education (CBE) DSM CB Non-university Public Dar es salaam
    iii.            Institute of Accountancy Arusha (IAA) IA Non-university Public Arusha.
     iv.            Institute of Finance Management (IFM) IF Non-university Public Dar es Salaam
       v.            Mkwawa University College of Education (MUCE) UDM University College Public Iringa
     vi.            Moshi University College of Cooperative and Business Studies (MUCCOBS) MC University College Public Moshi
   vii.            Mzumbe University (MU) MU University Public Morogoro
 viii.            Tanzania Institute of Accountancy (TIA) TA Non University Public Dar es Salaam
   ix.           Zanzibar Institute of Financial Administration (ZIFA) ZF Non-university Public Chwaka Zanzibar.

-ENGINEERING;
        i.            Ardhi University (ARU) AR University Public Dar es Salaam
      ii.            Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) DT Non-university Public Dar es Salaam
    iii.            Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) MB Non-university Public Mbeya
     iv.            Sokoine University of Agriculture (SUA) SU University Public Morogoro
       v.            St. Joseph College of Engineering & Technology (SJCET) JD Non University Private Dar es Salaam
     vi.            St. Joseph Institute of Information Technology (SJIIT) JS Non University Private Songea

 -ARTS
        i.            Community Development Training Institute Tengeru (CDTI) CD Non-university Public Arusha
      ii.            Institute of Social Work (ISW) SW Non-university Public Dar es Salaam
    iii.             Open University of Tanzania (OUT) OU University Public Dar es Salaam

 -EDUCATION;
        i.            Dar es Salaam University College of Education (DUCE) UDD University College Public Dar es Salaam
      ii.            Mwenge University College of Education (MWUCE) MW University College Private Moshi
    iii.            Sebastian Kolowa University College (SEKUCO) SK University College Private Tanga
     iv.            St Augustine University of Tanzania (Mtwara Centre) (SAUT) SAM University Center Private Mtwara
       v.            St Augustine University of Tanzania (SAUT) SA University Private Mwanza Tanzania Commission for Universities
     vi.            State University of Zanzibar (SUZA) SZ University Public Zanzibar
-MORE FACULTIES;
        i.            St John’s University of Tanzania (SJUT) SJ University Private Dodoma
      ii.            Institute of Rural Development Planning (IRDP) RD Non-university Public Dodoma
    iii.            Iringa University College (IUCO) IU University College Private Iringa
   iv.          Kampala International University Dar es Salaam Center (KIU) KU University Private Dar es Salaam
       v.          Makumira University College (MUCO) MK University College Private Arusha
     vi.           Mount Meru University (MMU) MM University Private Arusha
   vii.            Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) MN Non-university Public Dar es Salaam
 viii.            Ruaha University College (RUCO) RU University College Private Iringa
    ix.       St John’s University of Tanzania (SJUT) (Msalato Centre) SJM University Centre Private Dodoma
     x.         St John’s University of Tanzania (SJUT) (St Mark Centre) SJD University Centre Private Dar es Salaam
     xi.          Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCO) SM University College Private Moshi
   xii.          Teofilo Kisanji University (TEKU) TK University Private Mbeya
 xiii.          Tumaini University Dar es Salaam College (TUDARCO) TD University College Private Dar es Salaam
 xiv.            University of Arusha (UOA) UA University Private Arusha.
   xv.             University of Dar es Salaam (UDSM) UD University Public Dar es Salaam.
 xvi.            University of Dodoma (UDOM) DM University Public Dodoma.
   - Si hivyo tu ila pia kuna vyuo ambavyo havikujiingiza katika sual la TCU  kama chuo cha kiislam cha Morogoro (MUM),………………………..
Pia kwa maelezo zaidi ni vizuri kuingia katika website za vyuo vyenyewe (mfano MUHIMBILI UNIVERSITY)  kwani kuna maelezo ya kina zaidi ya haya na pia hata muda wa kozi, ada, lini fomu za kujiunga zinatoka na tarehe ya kurudisha pia. Pia unaweza kuingia katika website ya TCU wenyewe (www.tcu.go.tz) pia wanamaelezo kuhusuvigezo vya kujiunga na chuo, ada, muda wa kujisajili, namna ya kujisajili, pia vitu vinavyihitajika nk.

3. NAMNA YA KUJIUNGA KATIKA SECTA YA AFYA
-Katika suala hili ambalo ndio wazo kuu la uandishi wa nakala hii, tumeongelea upande wa afya hususani  katika chuo chetu cha MUHIMBILI.
Sababu kuu ni kutokana na udhalilishaji wa kijinsia ambao tunakutana nao katika mazingira yetu kikazi kwani utu haupo, mfano: wanaume huweza kufanyiwa vipimo na wanawake pia kwa baadhi ya sehemu wanawake hufanyiwa vipimo na wanaume.
Mifano hai ipo hususani kwa kinadada zetu au hata mama zetu pindi wapatapo ujauzito na kuhitaji msaada wa matibabu na  ni madhila mangapi wanayoyakuta.Hivyo kutokana na hilo tumeonelea ni bora sisi kama waislam   tuna dhimma ya kulinusuru hilo.
Hili ni kama jambo fardhi (kifaya) ambalo wachache wanaweza kufanya kwa ajili ya wengi, hivyo basi sisi hatuna budi kusoma ili tuwasaidie ndugu zetu kutokana na hali/tatizo  hili.
Kama ilivyoelezwa katika vipengele vilivyotangulia kuwa sio kupata matokeo mabaya kwani ndio mwisho wa ndoto zetu bali tuwe na ufahamu kuwa ziko namna / njia ambazo tunaweza kutumia ili tuweze kufikia malengo yetu.
Hivyo njia ambazo tunaweza kuzitumia hatimaye tuweze kutumiza malengo yetu ni kwa kutumia kozi fupi za awali kama diploma na hatimaye  tukaweza kuzifikia ndoto zetu, kama wanaotaka kuwa madaktari (specialist).
Hivyo mwisho kabisa tunaambatanisha na nakala ambazo zinaelezea kozi, muda wake ,alama zinazohitajika , na kazi ambayo wewe utaifanya kutokana na kozi hiyo ulivyo ichagua .
Kuhusu gharama zinazohusiana na  ADA , MALAZI , CHAKULA< MATIBABU,  na maelekezo mengine yanapatikana katika fomu ya kujiunga na chuo.
Fomu zetu za kujiunga na chuo cha afya  na tiba cha Muhimbili fomu zinapatikana chuo au kupitia katika website ya Chuo (www.muhas .ac.tz).

THE INSTITUTE OF ALLIED HEALTH SCIENCES IN A PUBLIC INSTITUTION FOR TRAINING MIDDLE LEVEL HEALTH CARE.

PROVIDERS TANZANIAN LEADING TO AWARD OF DIPLOMA AND ADVANCED DIPLOMA IN VARIOUS ACADEMIC.

PROGRAMMES.
The Institute is in position to provide in Tanzania learning, research and service in Allied Health Sciences that are based on curative, preventive, rehabilitative and restorative health care.

8.1.1 Diploma in Medical Laboratory Sciences
This is a six-semester Diploma in Medical Laboratory Sciences (DMLS) Programme. It intends to train health personnel capable of managing medical laboratory and diagnostic services focusing on preventive curative and rehabilitative health care. Students are also trained to carry out research activities relevant to provision of quality health in laboratory services.

8.1.1.1 Entry requirements
Direct Entry
Credits in Biology and Chemistry and one in either Physics or Mathematics at ‘O’ level.
Equivalent Qualifications
Laboratory Assistant with three years experience who has passed the selection examination recognized by the University and must have ‘O’ level secondary school certificate.

8.1.2 Diploma in Environmental Health Sciences
This is a six-semester Diploma in Environmental Health Sciences (DEHS) programme. It is intended to enable Environmental Health graduates to organize, plan, manage, supervise, monitor and evaluate, comprehensive preventive and promotional health services targeted at individuals and communities at all levels of the health care delivery system in the country and elsewhere. The programme is also intended to ensure that EHOs are provided with state of the art knowledge and skills, enabling them to be catalysts for sustainable and innovative health solutions by communities.

8.1.2.1 Entry requirements
Direct Entry
Pass in English and three credit passes, one in Mathematics and two other out of Physics, Chemistry and Biology at ‘O’ level.

Equivalent Qualifications
Health Assistant with three years experience who has passed the selection examination recognized by the University and must have ‘O’ level secondary school certificate.

8.1.3 Diploma in Diagnostic Radiography
This is a six-semester Diploma in Diagnostic Radiography (DDR) programme. The aim of the programme is to train radiographers to be able to use different kinds of X-rays CT IMRI ultrasound, CR and digital Radiography facilities scans and to investigate diseases injuries in patients. They should also be able to care for patients and maintain radiological facilities, i.e. Radiological and Imaging facilities in their place of work. The radiographer will also be trained to interpret plain radiographs and give intravenous injections where applicable.

8.1.3.1 Entry Requirements
Direct Entry
C grade or higher passes in three out of Physics, Chemistry, Biology and Mathematics and at least D grade pass in English. Physics is a major subject.
Equivalent Qualifications
Radiographer Assistant with three years experience who has passed the selection examination recognized by the University and must have ‘O’ - level secondary school certificate.
8.1.4 Diploma in Orthopaedic Technology
This is a Six-Semester Diploma in Orthopaedic Technology (DOT) Programme. The programme is intended to impart knowledge and skills to students on the evaluations, design, and fitting of different orthopaedic appliances, equipment and materials. It also aims to impart the correct attitude in students towards patient care.
8.1.4.1 Entry requirements
Direct Entry
Three credit passes out of Physics, Chemistry, Biology or Mathematics at O’level. Credit pass in engineering subjects is also acceptable as the third credit pass. Equivalent Qualifications Candidates must have certificate in lower limb Prosthetics or Orthotics and must have two credit passes in science subjects at “O” level.
8.1.5 Diploma in Pharmaceutical Sciences.
This is a Six Semester Diploma in Pharmaceutical Science (DPS) Programme. It is intended to train competent Pharmaceutical technician who can manage a district or a health care centre pharmacy under the supervision of a registered pharmacist. The training mainly focuses on imparting knowledge and skills to students on compounding and dispensing drugs to in-patient and out-patients in the health facilities. Also students are trained on providing drug related information to patients and the public at large.
8.1.5.1 Entry Requirement
Direct Entry
Three credit passes which must include Maths, Chemistry and English with a pass in Biology and Physics.

Equivalent Qualifications
Pharmaceutical Assistant with three years experience who has passed the selection examination recognized by the University and must have ‘O’ level secondary school certificate.

8.1.6 Diploma in Nursing
The Diploma in Nursing is an integrated training with midwifery and psychiatric nursing as options for which students choose but all of them get the training in general nursing. The training is of four academic years (8 semesters). Student’s progress is assessed by frequent tests during the semesters and at the end of the academic year. Fifty percent of the total marks is based on the results of the final examinations, the other 50% is from the continuous assessment tests.
8.1.6.1 Entry Requirements
i. Candidates must have completed O-level education with a credit in Biology and two passes in Chemistry and Mathematics or Physics.
ii. Candidates must have completed secondary school education within three years from the year of application.

8.1.7 Advanced Diploma in Nursing Education
This is a four-semester Advance Diploma in Nursing Education (ADNE) Programme. The programme intends to produce nurse teachers who will enhance the delivery of quality health education and health care in the country.

8.1.7.1 Entry Requirements
Direct Entry: N/A
Equivalent Qualifications
Registered Nurse with two years experience, who has passed the matriculation examination and must be a holder of ‘O’ level Certificate with credit/pass in Chemistry, Biology and English.

 8.1.8 Advanced Diploma in Dermatovenereology
This is a four Semester Advanced Diploma in Dermato-Venereology (ADDV) Programme. Students are trained to diagnose and competently manage most dermatological conditions, Leprosy, HIV/AIDS and other Sexually Transmitted diseases (STDs) in the context of Primary Health Care (PHC). The programme also intends to impart knowledge on how to plan and carry out appropriate measures for prevention of Skin diseases and STDs. Students are also trained to conduct operational research of both clinical and epidemiological nature and apply the findings in the improvement of health services in the community.
8.1.8.1 Entry Requirements
Direct Entry: N/A
Equivalent Qualification
Should have successfully completed any one of the following courses with an overall good performance grade(s).
- Assistant Medical Officer (AMO) in Tanzania In Other countries
- Medical Assistant
- Clinical Officer
- Nurse Clinician
- Family Nurse Practitioner Or an equivalent level, AND must possess ‘O’ level secondary school certificate with passes in Physics,Chemistry and Biology.
8.1.9 Advanced Diploma in Med. Lab. Sciences
This is a four-semester Advanced Diploma in Medical Laboratory Sciences (ADMLS) Programme.It intends to train health personnel capable of managing medical laboratory and diagnostic services focusing on preventive curative and rehabilitative health care. Students are also trained to carry out research activities relevant to provision of quality health in laboratory services.
Direct Entry: N/A
Equivalent Qualifications
Medical Laboratory technicians who hold a good Diploma in Medical Laboratory Sciences or its equivalent with two years working experience. Must possess ‘O’ level Secondary School Certificate with passes in Physics, Chemistry and Biology.

 HITIMISHO;
Tunamshukuru  Mwenyezimungu (s.w)  kwa kutuwezesha  sisi kuweza  kuiandika  na  kuiwakilisha  kwa  wenzetu  ambao  tunaona  kuwa kuna umuhimu  wa wao  kuyajua  mambo haya.
Pia  kwa upande mwingine  tunawashauri  ndugu zetu  waislamu.Sisi  ni katika wale wachache  ambao  tumechaguliwa  na Mwenyezimungu (s.w)  kuweza kuiendea  elimu  hii  ya sekula  nani wajibu kwetu  kusoma kwa ajili  ya kuwanusuru  waislamu wenzetu  na uislamu kwa ujumla.
Hivyo   ushauri sisi kama waislamu au wanafunzi wenzenu ni ;
v  Tuwe wajumbe  kwa wengine ambao wapo chini yetu ili tuweze kuuinua uislamu  na kuwanusuru waislamu wenzetu.
v  Tusibweteke (kujiamini)  kwa yale machache tunayoyajua.
v  Watu  wajitahidi kufuatilia habari baada ya  kumaliza elimu zao. Hii ni  ili kuweze kufikia katika kiwango cha juu zaidi  kielimu  na kuweze kutimiza ndoto zetu.
Kwa  mawazo, mchango, ushauri au lolote wasiliana nasi kwa;

ü   ABDALLAH ABDALLAH                   0784-560 920

ü  JUMANNE MASANJA                      0716-322 839

ü  MOHAMMED NYATI                       0785820012

ü  BAKARI  MSONGAMWANJA         0717-963 033

ü   SLIM                                                  0713-624 903

ü  BIWETE                                               0713-277 008

WABILLAHI TAWFIIK.