Thursday, December 13, 2012

KOREA KASKAZINI YAFANIKIWA KUTUMA ROKETI YAKE.


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini kurusha roketi angani, na kuionya nchi hiyo kwamba inaweza kuchukuliwa hatua kwa kile kilichoelezwa kuwa uchokozi, ambao umesababisha wasiwasi miongoni mwa marafiki na maadui  wake.

 Korea Kaskazini ililirusha roketi hilo jana, licha ya upinzani kutoka kwa mshirika wake wa karibu China. Ripoti kutoka Korea Kaskazini zinaeleza kuwa kuna furaha kubwa katika nchi hiyo inayoendesha mambo yake kwa siri kubwa, kutokana na mafanikio ya kurushwa kwa roketi hilo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura, baada ya kitendo hicho cha Korea Kaskazini, ambacho kimekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa namba 1718 na 1874 ambayo yanaikataza nchi hiyo kurusha makombora.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema mazungumzo yataanza mara moja kutafakari hatua ya kuchukuliwa. China, ambayo inayo kura ya turufu katika Baraza la Usalama, haikuashiria kama ingetoa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO