Wednesday, December 12, 2012

TAARIFA ZA DRONE YA MAREKANI ZAPATIKANA

Kamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, jeshi hilo limefanikiwa kupata taarifa zote zilizokuwemo kwenye ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani ambayo ilitekwa na Iran mwaka jana baada ya kuingia kinyemela katika anga ya Jamhuri ya Kiislamu. Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh amesema kuwa, Iran imefanikiwa kupata taarifa zote zilizokuwemo kwenye ndege hiyo ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ-170. 
DRONE RQ-170 IKIONYESHWA BAADA YA KUSHUSHWA NA WALINZI WA IRAN

Vile vile amesema kuwa, Iran imefanikiwa kugundua maeneo yote ambayo ndege hiyo ya Marekani ilitekeleza operesheni zake za kijasusi. Itakumbukwa kuwa Disemba 4, 2011, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitumia maendeleo yake ya kiteknolojia na kuilazimisha kutua chini ndege ya kisasa ya kijasusi ya Marekani baada ya kuingia kwa siri katika anga ya Iran na kuichukuwa ngawira. Brigedia Jenerali Hajizadeh pia amesema kuwa, Rais Barack Obama wa Marekani alikuwa amewaeleza viongozi wa utawala wa Kizayuni kwamba ndege hiyo ilikuwa inafanya ujasusi kwenye maeneo ya miradi ya nyuklia ya Iran lakini taarifa zilizopatikana ndani ya ndege hiyo zinaonyesha kuwa haikufanya operesheni hata moja kuhusu miradi ya nyuklia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO