Kituo ch televisheni cha taifa nchini Syria kimetangaza kuwa Rais Bashar al -Assad atatoa hotuba hii leo kuhusu vuguvugu linaloendelea la kuupinga utawala wake. Hotuba hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa Assad mwenye umri wa miaka 47 katika kipindi cha miezi kadhaa. Hii itakuwa mara ya kwanza pia kwa kiongozi huyo kuzungumza hadharani tangu alipotupilia mbali dokezo kwamba yumkini akenda kuishi uhamishoni ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini mwake ambavyo hadi sasa vimeshauwa watu 60,000. Hotuba ya Assad inakuja wakati waasi wakizidi kusonga mbele na mapambano ya kumuangusha madarakani ambapo sasa wamevitwaa baadhi ya vitongoji vya mji mkuu wa Damascus. Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Syria amekwenda Iran hapo jana kwa lengo la kuimarisha zaidi mahusiano na nchi hiyo ambayo ni mshirika mkubwa wa utawala wa Assad.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO