Baraza la Umoja wa Mataifa limeidhinisha matumizi  ya ndege zisizo na rubani, mashariki mwa Jamhuri  ya Kidemokrasi ya Kongo, baada wiki kadhaa za  ucheleweshwaji kufuatia wasi wasi wa Urusi, China  na Rwanda juu ya matumizi ya ndege hizo za  uchunguzi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ban  Ki-Moon aliliandikia Baraza hilo mwishoni mwa  mwezi uliyopita, kushauri kuwa walinda amani nchini  Kongo wanapanga kutumia ndege hizo kuboresha  uwelewa wa hali ya huko na kuharakisha mchakato  wa maamuzi katika kushughulikia uasi wa kundi la  M23. Rais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa  Januari, balozi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa  Masood Khan amemjibu Katibu Mkuu Ban kuwa  wamepokea maombi hayo na kuyaridhia. Lakini  baraza hilo limesema ndege hizuo zitatumika tu kwa  majaribio.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO