Tuesday, January 01, 2013

MAREKANI YAGEUZA HOTELI KITUO CHA KIJESHI


Marekani imeigeuza hoteli kubwa zaidi ya Sana'a, mji mkuu wa Yemen kuwa kituo cha kijeshi katika juhudi zake za kujaribu kupata eneo salama nchini humo baada ya mapinduzi ya wananchi yaliyomng'oa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Ali Abdallah Saleh.
Habari zinasema kuwa ubalozi wa Marekani mjini Sana'a umechukua vyumba vyote vya hoteli ya Sheraton na kuwafukuza wafanyakazi 200 wa hoteli  hiyo baada ya kuwalipa fedha zilizo sawa na mishahara yao ya miezi sita.
Mbali na kuwapa fedha hizo, ubalozi wa Marekani umeweka kamera za ujasusi katika hoteli hiyo na kuweka kikosi cha askari usalama karibu na jengo hilo. Marekani pia imeweka askari doria katika maeneo ya milimani ili kuilinda hoteli hiyo na wameamrishwa kufyatua risasi iwapo watashuku kitu chochote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO