Tuesday, January 01, 2013

NJAMA ZA KUIGAWA IRAQ ZAGUNDULIKA


Ahmad Sharifi, mtaalamu wa masuala ya kiistratijia nchini Iraq amesema kuwa Uturuki ikishirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel na Qatar zinafanya njama za kuigawa Iraq.
Sharifi amesema kuwa, serikali za Uturuki na Qatar zikishirikiana na utawala wa Israel zinapanga mikakati ya kutekeleza mpango wa Mashariki ya Kati mpya kwa kuuondosha mfumo wa kisiasa ulioko hivi sasa nchini Iraq na kuigawa vipande vipande nchi hiyo. Amemtaka Nouri al Maliki Waziri Mkuu wa Iraq kuchukua hatua za haraka za kuimarisha amani na utulivu nchini humo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira ya kuundwa serikali ya walio wengi ili kuzidhibiti taasisi za kiusalama nchini humo.
Hali ya kisiasa nchini Iraq ilichafuka baada ya kutiwa mbaroni walinzi wa Rafii al A'isawi Waziri wa Fedha wa nchi hiyo na kufuatiwa na maandamano dhidi ya serikali katika mkoa wa al Anbaa, ili kuishinikiza serikali ya Baghdad iwaachilie huru walinzi wake.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO