Uingereza, Ujerumani, Uholanzi na Australi  zimewataka raia wake kuondoka katika mji wa  Benghazi mashariki mwa Libya, kutokana na kitisho  dhidi ya raia wa nchi za Magharibi, kinachohusishwa  na kuingilia kijeshi kwa Ufaransa katika mgogoro wa  Mali. Onyo la Uingereza lililotolewa jana Alhamisi  liliikasirisha serikali ya Libya, iliyosema kuwa  hakukuwa na taarifa mpya za uchunguzi kuhalalisha  wasi wasi huo mjini Benghazi. Idara ya mambo ya  nje ya Australia imesema kuwa wanatambua tishio  maalumu kwa raia wa nchi za Magharibi mjini  Benghazi, na kuwataka raia wake kuondoka huko  mara moja. Waziri Mkuu wa Uingereza David  Cameron alionya wiki iliyopita kuwa kilichotoekea  nchini Algeria katika kiwanda cha gesi ni sehemu tu  ya vita virefu dhidi ya magaidi wauaji duniani kote.  Jana Alhamisi, Ujerumani na Uholanzi pia ziliwaonya  raia wake na kuwataka waondoke mara moja kutoka  Benghazi. Lakini naibu waziri wa mambo ya kigeni  wa Libya, Abdullah Massoud alielezwa kusikitisha  kwake juu ya onyo hizo, na kusema kuwa serikali  mjini Tripoli itahitaji maelezo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO