Monday, January 07, 2013

MURSI ASEMA WAZAYUNI WANAWANYONYA DAMU WAPALESTINA

Vyombo vya habari vya Misri vimesambaza video inayomuonesha Rais Muhammad Mursi akitoa matamshi makali dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2010 na kuwaita Wazayuni kuwa ni wafyonza damu na watu wenye uchu wa vita. Alisema hayo katika mahojiano ya mwaka 2010 aliyofanywa na televisheni ya al Quds inayorushwa hewani kutokea nchini Lebanon. Wakati huo Mursi alikuwa msemaji wa kundi la Ikhwanul Muslimin. Alisisitiza kuwa, mazungumzo ya amani na Israel ni kupoteza wakati na aliihesabu harakati ya "muqawama" kuwa njia pekee ya kuweza kuikomboa Palestina. Rais huyo wa Misri alidai pia kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina iliundwa na Wazayuni na Wamarekani maadui ili kuwadhibiti Wapalestina na kuwanyima haki zao. Alisema hakuna mtu yeyote mwenye busara ambaye anakubaliana na suala la kuendelea na njia hiyo. "Ima uwakubali Wazayuni na yote wanayotaka, au uingie vitani kupambana nao. Hivi ndivyo wanavyotaka wavamizi wa ardhi ya Palestina ambao ni wafyonza damu za Wapalestina, ni watu wenye uchu wa vita na ni wana wa sokwe na nguruwe," alisema. Wakati huo pia alitaka kuweko mapambano ya aina zote ya kijeshi, kisiasa na kiuchumi dhidi ya Wazayuni na kuwataka Waislamu duniani kuunga mkono "wanamuqawama" wa Palestina katika vita vyao vitakatifu. Aidha alipinga vikali mpango wa Waarabu wa kuwa na nchi mbili yaani Palestina na Israel na kusema kuwa, nchi ni moja tu nayo ni ya Wapalestina, katika ardhi ya Palestina yenye utambulisho na uraia wa Palestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO