Abdul Bari Laroussi, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Libya amesema kuwa, mgogoro wa mafuta katika kituo cha mafuta huko mashariki mwa Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo unaisababishia Libya hasara ya zaidi dola milioni moja kwa siku. Jana Jumamosi, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Libya alisema kuwa, mgomo huo wa wafanyakazi wa sekta ya mafuta katika kituo cha Zueitina unaisababishia Libya hasara ya dola milioni 1.3 kila siku.
Wafanyakazi wa kituo cha mafuta cha mashariki mwa Tripoli walianza mgomo tangu Disemba 23 mwaka jana na hivyo kukilazimisha kituo hicho kusitisha shughuli zake. Waziri wa Mafuta na Gesi wa Libya ameongeza kuwa, kusimamishwa kazi za za kituo hicho cha mafuta kumepelekea kukatwa kwa huduma za umeme pia katika baadhi ya maeneo ya Libya. Wafanyakazi kadhaa wa kituo cha Zueitina wakiwemo raia wawili wa kigeni wamejiuzulu kufuatia mgomo huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO