Wednesday, January 02, 2013

MWISHO WA ISRAEL UNAKARIBIA

Mshauri wa Rais Muhammad Mursi wa Misri, amesema kuwa, utawala haramu wa Kizayuni utasambaratika katika kipindi cha miaka 10 ijayo na amewataka walowezi wa Kizayuni kuanza kuhama huko katika ardhi za Palestina wanaozikalia kwa mabavu. Essam el-Erian ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimi nchini Misri amesema kuwa, Wazayuni walioloweya huko katika ardhi za Palestina wamekuwa ni tatizo kubwa la kurejea wakimbizi wa Palestina katika ardhi zao. Aidha amesema kuwa, aidiolojia ya Uzayuni imeshindwa kwani hadi hivi sasa imeweza kushawishi Wazayuni milioni sita tu kuhamia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wakati takwimu zinaonesha kuwa kuna Mayahudi milioni 14 katika kona mbalimbali za dunia. Amesema, kwa kuzingatia jambo hilo, anatabiri kuwa utawala wa Kizayuni utasambaratika katika kipindi cha miaka 10 ijayo. Siku mbili zilizopita pia Essam el-Erian aliwataka walowezi wa Kizayuni kurejea katika nchi walizotoka, suala lililopelekea kuzuka mjadala mkubwa nchini Misri.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO