Wednesday, January 02, 2013

MASHABIKI 60 WAFARIKI ABIDJAN


Watu wasiopungua sitini wamepoteza maisha baada ya kukanyagwa kanyagwa kwenye msongamano mkubwa wa watu katika uwanja wa michezo huko Abidjan mji mkuu wa Kodivaa. Imeripotiwa kuwa watu wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika msongamano huo uliotokea wakati wa sherehe za usiku wa kuamkia mwaka mpya wa 2013 Miladia.
Msemaji wa kikosi cha waokoaji kutoka Jeshi la Kodivaa Luteni Kanali Issa Sako amesema tukio hilo lilijiri mkesha wa mwaka mpya wakati idadi kubwa ya watu walipokusanyika kutazama maonyesho ya fataki.Amesema watu walikanyagwa na kukosea hewa wakati wakijaribu kuingia katika  uwanja huo mkuu wa Abdijan.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO