Wednesday, January 02, 2013

TALIBAN YASEMA MAREKANI INAELEKEA KUSHINDWA KAMA VIETNAM


Kundi la waasi la Taliban wameufananisha mpango wa Marekani kuondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan na ule wa kujiondoa kutoka Vietnam, na kuuita kuwa "tangazo la ushindi na mkakati wa kukimbia." Taarifa iliyotolewa na kundi hilo hivi leo, imesema kuhamishia operesheni za jeshi la Marekani kwa vikosi vya ulinzi vya Afghanistan, ni sawa na kushindwa kwa Marekani huko Vietnam ya Kusini, kabla ya ushindi wa Wakomunisti hapo mwaka 1975. 
Vikosi vya Jumuiya ya Kujihami ya NATO vinavyoongozwa na Marekani, vimepangiwa kuondoka nchini Afghanistan kufikia mwishoni mwa mwaka 2014. Hata hivyo, Marekani itabakisha kikosi kidogo nchini humo na mataifa mengine ya NATO yameahidi kuendelea kuisaidia serikali ya Afghanistan.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO