Ndege za kivita za Ufaransa zimeviharibu vituo viwili  vya wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa Mali,  wakati ambapo kuna ripoti kuwa waasi hao  wamegawanyika katika makundi mawili, moja likitaka  kufanya mazungumzo ili kukomesha mashambulizi  dhidi yao. Pia kumekuwepo na taarifa za majeshi ya  Mali kufanya mauaji ya kinyama, ambapo kundi moja  la haki za binaadamu limesema kuwa watu  wasiyopungua 31 waliuawa katika mji wa kati wa  Sevare, na maiti zao kutupwa katika visima. Chanzo  kutoka duru za jeshi kimesema kuwa mashambulizi  ya ndege yaliyofanyika usiku yamelenga vituo  vilivyoko Ansongo, kilomita 80 kutoka mji wa Gao, na  vituo vya kijeshi vya waasi vilivyoko katika kijiji jirani  cha Seyna Sonrai. Jana Alhamisi, kundi jipya  lililojitenga na Ansar Deen la Islamic Movement for  Azawad, lilisema katika taarifa yake kuwa linapinga  itikadi kali na ugaidi, na kwamba limedhamiria  kupambana navyo, na kuongeza kuwa linataka  suluhu ya muafaka ya mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO