Thursday, February 14, 2013

RUSSIA INAIUZIA SILAHA MALI

Shirika moja la Russia linalouza silaha kimataifa limesema limetuma shehena ya silaha nchini Mali na kwamba limepanga kutuma silaha zaidi katika nchi hiyo Kiafrika iliyotumbukia kwenye vita vinavyoongozwa na Ufaransa.
Anatoly Isaikin Mkurugenzi wa Shirika la Rosobornexpo amesema shehena ya kwanza ilitumwa wiki mbili zilizopita na mazungumzo yanaendelea kutuma shehena zingine ndogo ndogo. Ufaransa ilianzisha vita nchini Mali Januari 11 kwa kisingizio cha kupambana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. Nchi za Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zinaunga mkono hujuma hiyo inayoongozwa na Ufaransa nchini Mali.
Maelfu ya raia wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika wamelazimika kukimbia na kuyahama makazi yao baada ya vikosi vinavyoongozwa na Ufaransa kuingia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.
Weledi wa mambo wanaamini kuwa lengo kuu la Ufaransa katika vita vya Mali si kupambana na waasi bali ni kupora utajiri wa nchi hiyo kama vile mafuta ya petroli, dhahabu na madini ya urani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO