Thursday, February 14, 2013

ISRAEL IMEPORA DOLA BILIONI 480 UTAJIRI WA MISRI

Bomba la mafuta toka Misri hadi Israel
Waziri wa Mafuta wa Misri amesema Cairo itaushurutisha utawala haramu wa Israel kulipa gharama za utajiri wa Misri iliyoupora. Waziri wa Mafuta wa Misri Osama Kamal amenukuliwa akisema kuwa wakati utawala wa Kizayuni wa Israel ulipokalia kwa mabavu eneo la Sinai kuanzia mwaka 1976 hadi 1977, ulipora utajiri wa petrokemikali katika eneo hilo. Kwa mujibu wa wataalamu, petrokemikali yenye thamani ya dola bilioni 480 iliporwa na Israel katika eneo hilo. Kamal amesema Misri inapanga mkakati wa kuhakikisha kuwa utawala wa Kizayuni unashurutishwa kulipa dola bilioni 500 kama fidia ya utajiri huo. Ameongeza kuwa hivi sasa Misri imebatilisha mikataba ya kuiuzia Israel gesi asilia. Katika zama za dikteta wa Misri Hosni Mubarak aliyetimuliwa madarakani, Misri ilikuwa ikiizuia Israel gesi asilia kwa bei ya chini sana na hivyo kuwasababishia Wamisri hasara kubwa. Lakini baada ya mapinduzi ya wananchi wa Misri, nchi hiyo ilisitisha upelekaji gesi kwa utawala wa Kizayuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO