Kamanda wa ngazi za juu katika majeshi ya Iran
amesema hujuma yoyote ile ya Marekani, Saudi Arabia au nchi yoyote dhidi ya
mipaka ya baharini ya nchi hii itakabiliwa na jibu kali.
Mkuu wa Vikosi Vyote vya Kijeshi vya Iran Meja
Jenerali Firouzabadi amesema ndege za nchi za eneo zinaweza kupaa katika Ghuba
ya Uajemi na kwamba hakuna kizuizi cha kuruka katika maji ya kimataifa na hilo
halihesabiwi na Iran kuwa ni kitendo cha kichokozi. Matamshi ya Firiuzabadi
yamekuja baada ya Kamanda mwandamizi wa Marekani Jenerali James Mattis kukiri
kuwa vikwazo vinavyoongozwa na Marekani dhidi ya Iran vimefeli. Akizungumza
mbele ya Kamati ya Kijeshi ya Baraza la Seneti, Mattis alidai kuwa Marekani ina
njia kadhaa za kuilazimisha Iran isalimu amri. Kwa mara kadhaa sasa wakuu wa
Marekani na muitafaki wake mkuu, Israel, wamekuwa wakitoa vitisho dhidi ya Iran
mbali na kuiwekea nchi hii vikwazo vinavyokiuka sheria kwa kisingizio kuwa Iran
ina malengo ya kijeshi katika miradi yake ya nyuklia. Iran imekanusha vikali
madai hayo na kusema shughuli zake za nyuklia zinafanyika kwa malengo ya amani
na kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO