Mamilioni ya wananchi wa Venezuela wamejitokeza katika mji mkuu wa nchi hiyo
Caracas kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hugo Chavez aliyefariki dunia
siku ya Jumanne kutokana na maradhi ya kensa.
Umati mkubwa wa watu ilisindikiza mwili huo kwa zaidi ya masaa 6 hadi kufika
katika akademia ya jeshi ambako kiongozi huyo atazikwa kesho Ijumaa. Viongozi wa
America ya Latini tayari wameshawasili mjini Caracas kwa ajili ya kutoa heshima
zao za mwisho akiwemo Rais Cristina Fernandes de Kirchner wa Argentina, Jose
Mujica wa Uruguai, Evo Morales wa Bolivia na wengineo.
Nchi nyingi duniani zinaendelea kutuma risala zao za rambirambi na pole kwa
wananchi wa Venezuela kufuatia kifo cha rais Hugo Chavez. Rais Barack wa
Marekani hakutoa mkono wa pole bali ametoa risala fupi akitaka kufunguliwa
ukurasa mpya kuhusiana na utajiri wa mafuta ya nchi hiyo. Miongoni mwa masuala
yatakayokumbukwa kuhusiana na kiongozi hiyo mwanamapinduzi wa Venezuela ni
kuanzisha harakati ya mrengo wa kushoto iliyoenea katika eneo la Amerika ya
Latini ya kupinga ukoloni na ubeberu wa madola ya Magharibi hasa Marekani na
kupambana na umasikini.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO