Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa
UNICEF limeelezea wasi wasi wake kuhusu mateso dhidi ya watoto wa Kipalestina
wanaoshikiliwa katika jela za utawala haramu wa Israel. Katika taarifa yake UNICEF imetoa ratiba ya hatua
ambazo zitachukuliwa ili kuboresha hali ya watoto wa Kipalestina wanaozuiliwa na
jeshi la Israel. Kupitia taarifa yenye anuani ya "watoto walioko kwenye kizuizi
cha jeshi la Israel" UNICEF inapendekeza kutendewa vyema watoto wa Kipalestina
walioko kwenye kizuizi cha jeshi la Israel. UNICEF imesema watoto hao wanapaswa
kutendewa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya haki za watoto na vile vingine
vya kimataiafa. Ripoti hiyo ilitolewa baada ya kubainika kuwa watoto
wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za Israel wananyimwa haki zao. Imebainika
kuwa watoto wa Kipalestina wamekuwa wakitendewa vibaya wanapohojiwa au
wanapohamishiwa katika korokoro za utawala huo haramu. UNICEF inakadiria kuwa
kila mwaka watoto 700 wa Kipalestina wenye umri wa miaka 12 hadi 17 hukamatwa na
vikosi vya Israel na kufungwa gerezani kwa tuhuma ya kurusha mawe.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO