Thursday, March 07, 2013

ARAB LEAGUE YAWAPA WAASI NAFASI KATIKA JUMUIYA HIYO

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imeupa mrengo wa upinzani wa Syria unaoungwa mkono na nchi za Magharibi kiti cha serikali ya nchi hiyo katika jumuiya hiyo. Pia Arab League imeamua kuruhusu nchi wanachama kuwapatia silaha waasi wanaopigana dhidi ya Rais Bashar al Assad. Jumuiya hiyo imesema mrengo wa upinzani wa Syria utakalia kiti hicho hadi uchaguzi utakapofanyika nchini humo na kuundwa serikali mpya.
Jumuiya hiyo ya Kiarabu ilisimamisha uanachama wa Syria kwenye taasisi hiyo mwaka 2011 kwa madai kwamba serikali ya Rais Bashar al Assad ilishindwa kuheshimu mpango wa amani iliyoupendekeza kwa lengo la kuhitimisha mgogoro wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO