Rais mpya wa China,Xi Jinping amewasili mjini Moscow, Russia, mapema leo na kukutana na mwenyeji wake, Rais Vladmir Putin. Viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo mapana kuhusu jinsi ya kuimarisha ushirikiano wa kijeshi, kisiasa na kiuchumi. Rais Vladmir Putin kwenye mazungumzo hayo amesema Russia inatambua umuhimu wa China katika biashara na siasa za kimataifa na kwa mantiki hiyo, Moscow inaiona Beijing kama mshirika wake wa karibu katika masuala hayo.
Marais wa Russia na China pia wamesema wataendelea kutumia nafasi za nchi zao katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutetea haki za wanyonge na kudhibiti makeke ya wanachama wa baraza hilo ambao hutaka kushinikiza ulimwengu kwa maslahi yao ya kibinafsi. Inafaa kukumbusha hapa kuwa, Russia na China ni miongoni mwa nchi 5 wanachama wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Nchi zingine ni Marekani, Ufaransa na Uingereza.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO