Tuesday, March 05, 2013

OIC KUANZISHA MFUKO WA KULINDA DINI YA KIISLAM

Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC imetangaza kuwa imeamua kuanzisha mfuko wa fedha kwa ajili ya kutetea na kulinda dini ya Kiislamu na matukufu yake. Essam al Shant Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano cha OIC yenye makao yake huko Jeddah Saudi Arabia amesema kuwa jumuiya  hiyo inafanya juhudi za kuanzisha mfuko wa fedha kwa ajili ya kulinda na kuitetea dini ya Kiislamu, shaksiya na matukufu ya dini hiyo kwa kuungwa mkono na wanachama wake na pia na sekta binafsi. OIC imesema kuwa kufuatia pendekezo lililotolewa na Kuwait la kuasisi mfuko huo wa fedha, jumuiya hiyo hivi sasa inajiandaa kuunda timu ya ufuatiliaji kwa ajili ya kuainisha fedha zinazohitajika kwa ajili ya kuanzisha mfuko huo. Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa mfuko huo wa fedha ambao makao yake makuu yatakuwa nchini Kuwait ni mfuko wa wakfu na kwamba utakuwa ukitetea na kuilinda dini ya Kiislamu na matukufu yake pamoja na shakhsia wa Kiislamu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO