Tuesday, March 05, 2013

SAUDIA YAINGIA KIHOLELA ENEO LA MAFUTA LA YEMEN

Ripoti iliyotolewa na tovuti ya habari ya Shaharah inaeleza kuwa Saudi Arabia imeghusubu ardhi ya nchi jirani ya Yemen kufuatia kugunduliwa akiba kubwa ya mafuta katika eneo lililo karibu na mpaka wa pamoja wa nchi hizo. Afisa mmoja katika ofisi ya Rais wa Yemen amesema kuwa walinzi wa mpakani wa Saudia wameingia katia ardhi ya Yemen umbali wa kilomita tatu katika mkoa wa al Jawf huko magharibi mwa Yemen. Ameongeza kuwa Saudi Arabia mwezi Januari mwaka huu iliasisi pia vituo vinane vya upekuzi katika mpaka wake na Yemen chini ya mkataba wa Jeddah ambao ulitatua hitilafu za mpaka kati ya nchi hizo mbili za Kiarabu. Kwa mujibu wa mkataba huo, Saudi Arabia na Yemen zinapasa kukubali na kufanya mazungumzo yanayohitajika iwapo kutagunduliwa utajiri wa maliasi ya pamoja katika eneo la mpaka kati ya nchi mbili hizo ambayo inaweza kuchimbwa na kuwekezwa.  Hata hivyo kinyume na mkataba huo unavyosema hadi sasa Riyadh imekwepa kufanya mazungumzo na Sana'a na inaendelea kughusubu maeneo ya jangwani huko kaskazini mwa Yemen ambayo yana akiba ya mafuta na gesi ambazo hazijaanza kuchimbwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO