Zaidi ya mashirika 12 ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake kutoka mataifa ya kiarabu yameonya kuwa azimio la UN la kukabili unyanyasaji wa wanawake linatishiwa na upinzani kutoka kwa chama cha Muslim Brotherhood kutoka Misri, uongozi wa Vatican na Urusi. Azimio hilo liko katika hatua za mwisho za mashauriano kabla ya kuidhinishwa na tume ya kutetea maslahi ya wanawake katika Umoja huo.
Muslim Brtoher hood imesema kuwa azimio hilo linatishia kuvuruga mpangilio katika jamii kwa kuwapa wanawake ruhusa ya kusafiri, kufanya kazi au hata kupanga uzazi bila idhini ya waume wao.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO