Saturday, April 06, 2013

ASSAD AONYA KUHUSU KUANGUKA UTAWALA

Rais wa Syria, Bashar al-Assad, ameonya kuwa kuanguka kwa utawala wake kutadhoofisha eneo la Mashariki ya Kati kwa miaka mingi. Onyo hilo amelitoa wakati ambapo Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kufanya mazungumzo na nchi washirika wa Mashariki ya Kati kuhusu mzozo huo. Akizungumza katika mahojiano na vyombo vya habari vya Uturuki, yaliowekwa katika ukurasa wa Rais Assad wa mtandao wa kijamii wa Facebook, amesema dunia nzima inajua iwapo Syria itagawanyika na vikosi vya kigaidi kuchukua madaraka ya nchi, hali kama hiyo moja kwa moja itatokea katika nchi jirani. Kutokana na kuendelea kwa mapambano kati ya waasi na vikosi vya serikali na kuongezeka kwa mzozo wa kibinaadamu, Rais Obama atafanya mazungumzo na viongozi wa Jordan, Uturuki, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu katika wiki zijazo, kujadiliana kuhusu mzozo wa Syria ulioingia mwaka wake wa tatu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO