Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Marekani kuifunga jela ya Guantanamo. Navy Pillay ameongeza kuwa, kuendelea kushikiliwa idadi kadhaa ya watuhumiwa kwenye jela ya Guantanamo, kunakinzana wazi na sheria za kimataifa. Pillay amesisitiza kuwa, kushikiliwa watuhumiwa hao bila ya kufahamika makosa yao au kuhukumiwa, kunakinzana na sheria za kimataifa. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, karibu nusu ya mahabusu 166 wa jela ya Guantanamo wamepokea vibali vya kuhamishiwa kwenye nchi zao walikozaliwa au kwenye nchi nyingine ya tatu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, jela ya Guantanamo ilianza mwaka 2002 mara baada ya shambulio la Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, kwa shabaha ya kuwashikilia watuhumiwa wa vitendo vya kigaidi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO