Monday, April 29, 2013

GENGE LA MAGAIDI LAKAMATWA IRAQ

Maafisa usalama wa Iraq wamekamata genge la magaidi baada ya kushindwa katika jaribio la kumuua afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika wilaya ya al Adl mjini Baghdad. Magaidi hao walitaka kumuua afisa huyo kwa kutumia silaha zisizotoa sauti. Tukio hilo limejiri baada ya Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki kutahadharisha juu ya njama za kutaka kuirudisha nchi hiyo kwenye vita vya ndani. Mikoa kadhaa nchini huko inashuhudia makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wanajeshi na wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida na chama cha Baath.
Katika upande mwingine maafisa wa usalama wa Iraq wametangaza kuwa, watu karibu 20 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika milipuko mitatu ya kutegwa kwenye magari. Milipuko miwili kati ya hiyo imetokea kwa kufuatana katika mji wa Amara ulioko kilometa 200 kusini mashariki mwa mji mkuu Baghadad na mlipuko wa tatu umetokea kwenye mji wa Diwaniya kusini mwa Baghdad

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO