Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel, Binyamin Ben-Eliezer, amedai kuwa  silaha za kemikali za Syria zinamiminika kwa kundi la wapiganaji la Hezbollah.  Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mwanasiasa wa ngazi ya juu wa Israel.  Ben-Eliezer, ambaye pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati vita vya  wenyewe kwa wenyewe vya Syria na kumaliza mauaji ya raia, hakueleza ni  wapi amepata ushahidi huo. Amesema mchakato wa kusafirisha silaha  kwenda kwa Hezbollah, umeanza, ingawa amekataa kutoa ufafanuzi zaidi.  Israel imerudia kuelezea wasiwasi wake kwamba silaha za kemikali za Syria,  huenda zikaangukia mikononi mwa wapiganaji wanaoipinga Israel kama vile  kundi la Hezbollah la Lebanon au kundi lenye mafungamano na mtandao wa  kigaidi wa Al-Qaeda, linalopigana na waasi wanaopambana na serikali ya  Rais Bashar al-Assad.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO