Mkuu wa Umoja wa Usafirishaji Nje Vifaa vya Tiba wa Iran amesema kuwa, zaidi ya mashirika 20 ya Kiirani yanayotengeneza vifaa mbalimbali vya tiba vikiwemo vya matibabu ya meno na vifaa vya maabara yanasafirisha nje vifaa hivyo kwa zaidi ya nchi 70 duniani.
Bw. Abdu Ridha Yaakubzadeh amesema kuwa, vikwazo vya nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani vimetoa fursa kwa vijana wa Kiirani kutumia vipaji vyao kujiimarisha kielimu na hivi sasa mashirika ya Iran yanauza vifaa vya kisasa vya tiba kwa zaidi ya nchi 70 huku kila shirika likiwa linaingiza zaidi ya dola milioni 10 kila mwaka.
Vile vile amesema juhudi zinafanyika ili kuzidi kuyatangaza ulimwenguni maendeleo hayo makubwa ya kiyasansi ya Iran.
Itakumbukwa kuwa, maonyesha ya 16 ya vifaa vya tiba, maabara, madawa na huduma za afya yatafanyika tarehe 18 hadi 21 mwezi ujao wa Mei hapa mjini Tehran.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO