Tuesday, April 09, 2013

MAJASUSI WATIWA NGUVUNI NA PALESTINA

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa vikosi vya usalama vya HAMAS vimewatia mbaroni watu kadhaa katika Ukanda nwa Ghaza wanaoshukiwa kuwa majasusi wa mashirika kadhaa ya ujasusi ya nchi za Magharibi na Kiarabu. Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani wa serikali halali ya Palestina inayoongozwa na harakati ya Hamas imemnukuu Mohammed Lafi, mkuu wa usalama wa ndani akisema kuwa, nusu ya majasusi hao wamekiri kuwa wamekuwa wakifanya vitendo vya kijasusi kwenye ukanda huo. Lafi amewaonya Wapalestina wengine wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya kuyapatia taarifa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi. Itakumbukwa kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani wa serikali ya Hamas katikati ya mwezi Machi mwaka huu iliwaonya wale wote wanaoufanyia ujasusi utawala wa Kizayuni kwamba watasakwa bila ya huruma iwapo hawatajikabidhi kwa vyombo husika hadi kufikia Aprili 11.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO