Friday, April 05, 2013

KAMATI NIGERIA KUJADILI KUWASAMEHE WANACHAMA WA BOKO HARAM

Serikali ya Nigeria imeunda kamati maalumu ambayo imepewa jukumu la kuchunguza uwezekano wa kuwasamehe wanachama wa kundi la Boko Haram.  Kamati hiyo ambayo imeandwa jana baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa inatakiwa ichunguze kwa makini uwezekano pamoja na faida za kusamehewa wanachama wa Boko Haram. Taarifa zaidi zinasema kuwa, kamati hiyo inayosaidiwa na mshauri ya Rais Goodluck Jonathani katika masuala ya usalama ina muda wa majuma mawili kuchunguza pande za kadhia nzima ya kusamehewa wanachama wanaobeba silaha wa Boko Haram na kutoa ripoti kuhusiana na suala hilo. Kundi la Boko Haram limehusika katika milipuko na mashambulizi tofauti katika miji kadhaa ya Nigeria tangu mwaka 2009.  Mamia kwa mamia ya watu wameuawa katika mashambulizi ya kundi hilo lenye misimamo ya kufurutu ada, tangu lilipoanzisha mashambulio yake nchini humo mwaka 2009.
 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO