Saturday, April 06, 2013

URUSI YAOMBWA NA KOREA KUONDOA MABALOZI WAKE

Ujerumani imemwita Balozi wa Korea Kaskazini mjini Berlin leo, kulalamika juu ya kuzidi kwa hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea, ikisema ni kosa la Korea Kaskazini. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje mjini Berlin alisema balozi huyo aliitwa katika Wizara hiyo na kuelezwa bayana juu ya wasiwasi wa serikali ya Ujerumani. Alisema vitendo vya Korea Kaskazini havikubaliki hata kidogo si kwa matamshi wala mantiki, na kwamba Ujerumani ina matumaini mawaziri wa kigeni wa kundi la nchi nane za viwanda watatoa jibu sahihi na la pamoja wakati wa mkutano wao mjini London, wiki ijayo. Wakati huo huo, Korea ya Kaskazini imeitaka Urusi kufikiria uwezekano wa kuwaondoa wafanyakazi wa ubalozi wake mjini Pyongyang kutokana na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika Rasi ya Korea. Hata hivyo, msemaji wa ubalozi huo amesema licha ya kulipokea ombi hilo, bado Urusi haijapanga kuwaondoa wafanyakazi wake nchini Korea ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO