Sunday, April 07, 2013

KERRY AOMBOLEZA VIFO VYA WAMAREKANI


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry leo ameomboleza kifo cha kwanza cha mwanadiplomasia wa Marekani kuuawa akiwa kazini, tangu kutokea kwa shambulio la Septemba mwaka uliopita kwenye ubalozi wa Marekani mjini Benghazi, Libya.
Akizungumza na wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani mjini Istanbul, Uturuki, Kerry amesema kifo cha mwanadiplomisia huyo, Anne Smedinghoff kinakumbusha hatari inayowakabili wafanyakazi wa Marekani walioko nje.
Anne ni miongoni mwa Wamarekani sita waliouawa katika shambulio la jana nchini Afghanistan.
Alipoanza kazi tu, Kerry ambaye kwa sasa yuko ziarani nchini Uturuki, aliahidi kuwa jambo la kipaumbele ni kuwalinda wanadiplomasia wa Marekani. Suala hilo limekuwa nyeti sana tangu aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya, Chris Stevens na Wamarekani wengine watatu kuuawa katika shambulio la Benghazi. Hakuna mtu yeyote aliyefikishwa mbele ya sheria kutokana na shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO