Takribani wajumbe mia nne wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya msaada na serikali mbalimbali wamekutana kwa lengo la kuisaidia Darfur kurejea katika mkakati endelevu wa kujikwamua kijamii. Waziri wa maendeleo ya kimataifa Lynne Featherstone kutoka Uingereza alibainisha kuwa mkutano huo unawapa fursa kubwa watu wa Darfur kupata uungwaji mkono wanaohitaji ili kuepuka vita na utegemezi wa misaada ya dharura.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO