Tuesday, April 09, 2013

KOREA KASKAZINI YAFUNGA KIWANDA CHA PAMOJA NA KOREA KUSINI

Korea ya Kaskazini imesitisha mradi wa mwisho wa pamoja na Korea ya Kusini, baada ya wiki kadhaa  za vitisho dhidi ya Marekani na Korea ya Kusini kwa kufunga eneo la viwanda la Keosong na kuwaondoa wafanyakazi wake wapatao elfu 50. Kumekuwa na hofu kuwa Korea ya Kaskazini itafanya jaribio la kinyuklia na kuwa tishio kuu katika Rasi ya Korea tangu kumalizika kwa vita vya Wakorea mwaka 1953. Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema mzozo wowote wa kinyuklia sasa utafanya mkasa wa kuvuja kwa mionzi ya nyuklia huko Chernobly kuonekana hadithi za kitoto. Umoja wa Mataifa umesema Korea ya Kaskazini haiwezi kuendelea na vitisho vyake na kukiuka mamlaka ya Baraza la Usalama la Umoja huo na jamii ya kimataifa. Wizara ya mambo ya nje ya China imesema inataka kuona amani katika rasi hiyo na kuzitolea wito pande zote mbili husika kushughulikia tafauti zao kupitia mazungumzo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO