Korea ya Kusini imesema itawaondoa wafanyakazi wake wote kutoka  eneo la viwanda inalolimiliki pamoja na Korea ya Kaskazini. Uamuzi  huo umefikiwa baada ya Korea ya Kaskazini kutupilia mbali  pendekezo la Kusini, kuhusu mazungumzo juu ya kuanza tena kazi  katika eneo hilo la viwanda la Kaesong. 
Jana Korea ya Kusini iliipa Kaskazini muda wa masaa 24 kukubali  pendekezo hilo, na kuonya kuwa endapo litakataliwa ingechukua  hatua muhimu ambazo hata hivyo ilikuwa haikuzitaja. Eneo la  viwanda la Kaesong linatoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 53 elfu  katika kampuni 123 za Korea ya Kusini. Eneo hilo ambalo liko umbali  wa kilomita 10 ndani ya Korea ya Kaskazini, ni mfano adimu wa  ushirikiano kati ya nchi hizo. 
Korea ya Kaskazini iliwaondoa wafanyakazi wake wote tarehe 9  Aprili na kusimamisha shughuli zote, kudhihirisha hasira zake dhidi  ya kauli ya Korea ya Kusini kwamba ingepeleka wanajeshi kulinda  raia wake katika eneo hilo.  
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO