Sunday, April 07, 2013

MAREKANI YAAKHIRISHA JARIBIO LA KOMBORA LAKE

Afisa wa Marekani, amesema nchi hiyo itachelewesha jaribio la kombora la masafa marefu, kutokana na mvutano na Korea Kaskazini. Amesema, Waziri wa Ulinzi, Chuck Hagel, ameamua  jaribio hilo lifanyike mwezi Mei na sio wiki ijayo kama ilivyokuwa imepangwa. Korea Kaskazini, ambayo ilikasirishwa na vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa na ushirikiano wa kijeshi wa Marekani na Korea Kusini katika rasi ya Korea, imekuwa ikitoa vitisho katika wiki za hivi karibuni. Mwezi Februari, nchi hiyo ilifanya jaribio la nyuklia hatua iliyosababisha kuwekewa vikwazo vipya mwezi Machi. Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un amesema nchi yake haiwezi kuhakikisha usalama wa mabalozi baada ya Jumatano ijayo. Hata hivyo, serikali nyingi, ikiwemo Ujerumani zimesema balozi zao nchini humo, kwa sasa zinaweza kuendelea na majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO