Mtanadao wa
wadukuzi wa mtandao (Hakers) wanaojulikana kwa jina la “Anonymous”, wametoa
taarifa fupi kupitia mtandao wa “Tweeter” na kurusha video fupi kwenye mtandao
wa “Youtube” kuwa wameweza kudukua websites zaidi ya 700 za utawala haramu wa
Israel. Anonymous wamefanya hivyo ili kuwaunga mkono wapalestina wanaoonewa
huko Gaza. Anonymous wanadai kuwa dunia imekaa kimya na kuona damu ikimwagika
huko gaza kwa mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel bila hatua zozote
za kisheria kuchukuliwa dhidi ya utawala huo. Taarifa yao fupi, anonymous
wanasema “wataalamu wa mtandao kutokea sehemu mbalimbali za dunia wameamua
kuungana na kuwaunga mkono wapalestina dhidi ya waisraeli kwa kuwaondoa
waisraeli katika ulimwengu wa mtandao”. Wanaendelea kusema katika taarifa yao, “Mmeshindwa
kusimamisha hujuma dhidi ya haki za binaadamu, Mnakalia makazi ya wapalestina
kimabavu, Hamjaacha kuheshimu kusimamisha vita na mnaendelea kuonesha dunia
kuwa hamuheshimu sheria za kimataifa”.
Mitandao iliokuwa
imedukuliwa ni pamoja na mitandao ya benki, shule, biashara na hasa mitandao ya
serikali. Mitandao mingi ya Israeli leo haikuwa ikifanya kazi, na kila
utakapoifungua basi utapata taarifa fupi inayosema “Page cannot be displayed,
the system cannot communicate with the external sever…………..”
Tazama video hii walioirusha kupitia mtandao wa “youtube”.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO