Sunday, April 07, 2013

MELI ZA KIVITA ZA IRAN ZAELEKEA GHUBA YA ADEN

Msafara wa 25 wa meli za kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeelekea katika Ghuba ya Aden na maji wa kimataifa. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, msafara huo uling'oa nanga kutoka kusini mwa Iran baada ya kurejea msafara wa 24 wa meli za kivita za Iran ambazo zilikuwa zinalinda doria katika maji ya kimataifa.
Msafara huo wa 25 wa manowari za Iran unajumuisha meli ya kilojistiki ya Lark na meli ya kivita ya Alborz. Manoari hizo zitatia nanga katika bandari za nchi kadhaa rafiki. Msafara wa 24 wa manoari za Iran zilipita katika Lango Bahari la Malacca katika Bahari ya Pasifiki na kufika hadi China. Jeshi la wanamaji la Iran limeimarisha harakati zake katika maji ya kimatiafa kwa lengo la kulinda doria na kusindikiza meli za Iran na za kigeni katika maji hayo. Katika fremu ya juhudi za kimataifa za kukabiliana na maharamia, Jeshi la Wanamaji la Iran limekuwa likilinda doria katika Bahari Hindi na Ghuba ya Aden tokea Novemba mwaka 2008.  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza juhudi na mafanikio ya Iran katika kupambana na maharamia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO