Jenerali Pervez Musharraf rais wa zamani wa 
Pakistan ametiwa mbaroni kuhusiana na kesi ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa 
nchi hiyo Benazir Bhutto. Musharraf anatuhumiwa kula njama za mauaji ya Bi. 
Butto aliyefariki dunia katika shambulizi lililotokea Disemba mwaka 2007. 
Imeelezwa kuwa, Musharraf anaendelea kubakia nyumbani wake mjini Islamabad 
anakoshikiliwa kwenye kifungo cha nyumbani kutokana na uamuzi wake wa kuwatimua 
kazi majaji Novemba mwaka 2007 alipotangaza hali ya hatari nchini humo.
Kukamatwa kwake pamoja na kukosa sifa za kugombea 
uchaguzi wa Mei 11 vimetoa pigo kubwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi wa 
Pakistan, ambaye alirejea nchini humo mwezi uliopita akiahidi kile alichokiita 
kuwa ni 'kuiokoa' nchi. Inafaa kushiaria hapa kuwa, hadi sasa hakuna hata mtu 
mmoja aliyepatikana na hatia au kuhukumiwa kutokana na mauaji ya Bi. Benazir 
Bhutto, ijapokuwa kesi hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu sasa.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO