Friday, April 26, 2013

NATO YASEMA IMEFANIKIWA AFGHANISTAN


Majeshi ya jumuia ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO imesema kuwa vita dhidi ya Wanamgambo wa Taliban imeshinda nchini Afghanistani ingawa kumekuwepo na Ripoti za Mashirika mengine kuwa Mashambulizi ya Wanamgambo yameongezeka mwaka huu. Jenerali wa majeshi ya ISAF Joseph Danford amesema kuwa ingawa kumekuwepo na changamoto kadhaa lakini hali ya usalama imeimarika nchini Afghanistani. 
Miongoni mwa Mafanikio yaliyoidhinishwa ni pamoja na kuwawezesha watoto takriban Milioni nane wamekwenda shuleni asilimia 40 wakiwa Wasichana, ikilinganishwa na Watoto Milioni moja ambao wengi wao Wavulana walikwenda shule chini ya utawala wa Taliban wa mwaka 1996-2001. Hivi sasa imeelezwa wanawake wanashikilia zaidi ya asilimia 25 ya viti vya Ubunge halikadhalika Wanawake pia wameanza kujitokeza na kujiunga na Jeshi la Afhanistani.
Kwa Mujibu wa Takwimu za Shirika la utafiti lisilo la Kiserikali Mashambulizi ya Taliban na Wanamgambo wengine yameelezwa kuongezeka tangu mwezi Januari mapaka March mwaka huu ikilinganishwa na kipindi hicho hicho kwa mwaka uliopita. Umoja wa Mataifa umeripoti kuongezeka kwa Mashambulizi kwa na kusababisha madhara kwa Raia kwa asilimia 30 katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Machi mwaka huu.
Kamanda wa majeshi ya ISAF amesema kuwa Operesheni bado inaendelea na kuwa Wanamgambo watapamabana na Majeshi ya Afghanistani na Polisi wa nchi hiyo ambao bado wanaendelea kujiimarisha. Wanajeshi 100,000 wa ISAF watamaliza Operesheni yao mwishoni mwa mwaka 2014 na hivi sasa Vikosi vya kigeni viemanza kuondoka kwa awamu huku Majeshi ya Afghanistan yakitarajiwa kubeba Jukumu la kulinda usalama wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO