Duru za habari nchini Brazil zinaarifu kuwa, polisi 23 wa nchi hiyo 
wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha, kwa kosa la kuwaua wafungwa nchini 
humo. Kwa mujibu wa habari hiyo polisi hao waliohukumiwa kila mmoja kifungo cha 
miaka 156, walihusika katika mauaji makubwa zaidi dhidi ya wafungwa 111 katika 
jela moja ya nchi hiyo mnamo mwaka 1992. Aidha polisi hao 23 ni miongoni mwa 
polisi 26 ambao walihukumiwa hapo jana na kuachiliwa huru watatu kati yao. 
Maafisa hao wa polisi ambao wengi wao tayari walikuwa wamestaafu, walihusika 
katika mauaji ya wafungwa katika jela ya Carandiru iliyopo katika mji wa Sao 
Paulo mwaka huo uliotajwa. Hata hivyo mawakili wa polisi hao walioitaka mahakama 
ya Sao Paulo kuwapunguzia adhabu wateja wao, walidai mahakamani kuwa, polisi hao 
waliwafyatulia risasi wafungwa hao baada ya maisha yao kuwa hatarini.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO