Rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa amekubali
matokeo ya mkutano wa dharura wa viongozi wa eneo hilo ambao wameafikiana
kutotambua rasmi uongozi wake.
Mkutano huo uliofanyika nchini Chad ulimtaka bwana Mitchel Djotodia aunde
baraza la mpito kusimamia nchi hiyo na kuandaa uchgauzi katika miezi kumi na
nane ijayo. Awali wanajeshi wake waasi walipotwaa uongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, na
kumfukuza aliyekuwa rais Francois Bozize, bwana Djotodia alisema kuwa hata achia
mamlaka hadi atawale miaka mitatu.
Wakati huo huo, nchi Jirani ya Chad imekanusha madai yaliyotolewa na rais
aliyeondolewa mamlakani Francoise Bozize, kwamba nchi hiyo iliwasaidia waasi
kupindua serikali yake. Waasi wa Seleka walivamia mji mkuu Bangui na hatimaye kumfurusha rais
Francoise Bezize kutoka kasri lake mwezi mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO