Wednesday, April 10, 2013

UTURUKI WAITAKA NATO IWAPE NAFASI

Wakazi wa mji wa Istanbul, Uturuki wameandamana na kulitaka shirika la kijeshi la Nato kuondoka nchini humo. Waandamanaji hao ambao walikusanyika katika maidani ya Galatasarai  kufuatia wito uliotolewa na muungano wa  kupambana na ubepari na Nato unaoundwa na taasisi kadhaa zisizo za kiserikali walikuwa wakipiga nara dhidi ya Nato na ubepari na kulitaka shirika hilo la kijeshi kuondoka huko Uturuki. Msemaji wa wafanya maandamano hayo Basr Uzgur amesisitiza kuwa wananchi wa Uturuki hawataki kuwepo wanajeshi wa Nato na kuongeza kuwa wananchi katika eneo hawataki vita na kwamba Waturuki pia wanaipinga Nato na ubepari.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO