Sunday, May 05, 2013

KERRY AKOSOLEWA KWA KUWAPUUZA WAPALESTINA

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa juhudi za Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kuhusiana na kadhia ya Palestina hazina nia ya dhati na ya kweli ya kutatua suala la Palestina kwa njia za kiadilifu. Khalid Mash'al amesema kuwa, safari ya hivi karibuni ya John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani katika Mashariki ya Kati ilifanyika katika fremu ya kuunga mkono siasa za kupenda kujitanua za utawala ghasibu wa Israel. Mash'al ameongeza kuwa, inasikitisha kwamba, katika safari yake hiyo, Kerry hakuushinikiza hata kwa maneno utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unazikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina. Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa tena kushikilia wadhifa wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Bwana Khalid Mash'al amesema bayana kwamba, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani hajapendekeza mpango wowote wa kutatuliwa kadhia ya Palestina kwa njia za kiadilifu na hii inaonesha jinsi asivyokuwa na nia ya dhati kuhusiana na kupatiwa ufumbuzi kadhia ya Wapalestina na Wazayuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO