Tuesday, June 11, 2013

HALI YA MANDELA BADO TATA

Habari kutoka Afrika Kusini zinasema kuwa, hali ya kiafya ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela bado si nzuri licha ya kuwa hospitalini kwa siku ya tatu mfululizo. Taarifa ya serikali ya Pretoria imesema hali ya Mandela ambaye pia anafahamika kwa jina la Madiba bado haijabadilika ingawa mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel anapumua mwenyewe. Mandela aliongoza mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na kuwa rais wa kwanza mweusi nchini humo mwaka 1994. Kiongozi huyo wa zamani anayeenziwa zaidi duniani amekuwa akilazwa hospitalini mara kadhaa kutokana na maambuziki kwenye mapafu yake. Duru za karibu na Madiba zinasema kuwa, umri wake mkubwa (94) ni miongoni mwa sababu zinazomfanya alemewe ki afya kwani viongo vyake muhimu havina nguvu ya kutosha ya kuhimili maradhi. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amewataka watu wote nchini humo na duniani kwa ujumla kumuombea mzee Mandela ili apate nafuu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO