Saturday, June 15, 2013

IDB KUISAIDIA TUNISIA

Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (IDB) imetangaza kuwa, itaipa msaada wa fedha kwa serikali ya Tunisia. Benki hiyo imetangaza kuwa, itaipatia serikali ya nchi hiyo mkopo na msaada usio na masharti wenye thamani ya dola bilioni moja na milioni 200. Waziri Mkuu wa Tunisia Ali Laarayedh amesema kuwa, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa, fedha hizo zitakabidhiwa kwa serikali ya nchi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu. Amesema kuwa, fedha hizo zitatumika katika kutekeleza mipango mbalimbali ya sekta ya kilimo viwanda na biashara. Wakati huo huo, duru za habari kutoka Tunisia zinaarifu kuwa, Wairani waishio nchini humo mapema leo, wamefika kwenye masanduku ya kupigia kura ili kumchagua Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa hamasa kubwa. Habari zinasema Wairani hao waliwasili majira ya saa mbili asubuhi kwenye ubalozi wa Iran mjini Tunis na kushiriki katika zoezi hilo muhimu la duru ya 11 ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO