Mjumbe moja wa Kamati ya Utendaji ya Kituo cha Uchaguzi nchini Iran amesema kuwa, hadi anatangaza habari hiyo, zaidi ya asilimia 70 ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura walikuwa tayari wameshiriki katika duru ya 11 ya uchaguzi wa rais na duru ya nne ya uchaguzi wa mabaraza ya miji na vijiji hapa nchini.
Bw. Ismail Kauthari ameongeza kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi zaidi mikoani na vijijini.
Hadi tunapokea habari hii, upigaji kura ulikuwa unaendelea na ulikuwa tayari umeshaongezewa muda kwa mara kadhaa jambo ambalo linaonesha wazi kuwa asilimia ya watu walioshiriki kwenye zoezi hili muhimu itakuwa kubwa zaidi ya hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO